Nguzo tano za Uislamu ni mfumo wa maisha ya Muislamu. Ndizo ushahidi wa
Imani, Swalah, utoaji wa Zakaah (kuwasaidia wernye dhiki), kufunga
katika mwezi wa Ramadhaan na kuhiji Makkah mara moja maishani kwa wale
wenye uwezo
1) Shahada ya Imani

Mahujaji wakiswali katika Msikiti wa Haram huko Makkah. Msikitini humu mna Ka’abah (jengo jeusi linaloonekana katika picha) ambalo Waislamu hulielekea wakati wakiwa katika Swalah. Ka’abah ni mahali pa ibada ambapo Mwenyezi Mungu Aliwaamuru Mitume Ibraahiym na mwanaye, Isma’iyl waijenge.
Ibada za hija ni pamoja na kuitufu Ka’abah mara saba na kwenda mchakamchaka baina ya kilima cha Swafa na Marwa mara saba, sawa na Hajar alivyofanya wakati akitafuta maji. Kisha, Mahujaji husimama pamoja katika uwanja wa ‘Arafah[112]na kumwomba Mwenyezi Mungu wakipendacho na kwa ajili ya maghufira, katika kile ambacho mara nyingi hufikirika kuwa ni onyesho la awali la Siku ya Malipo.
1) Shahada ya Imani
Ushahidi wa Imani ni kusema kwa kusadikisha, “La ilaaha illAllaah, Muhammadur Rasulullah.” Maana ya matamshi haya ni, “Hapana
mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (Allaah), na
kwamba Muhammad ni Mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.” Sehemu
ya kwanza, “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki, isipokuwa Mwenyezi
Mungu,” inamaanisha kwamba hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa
Mwenyezi Mungu peke Yake, na kwamba Yeye hana mshirika wala mwana.
Ushahidi huu wa Imani unaitwa Shahada, ambayo ni kanuni
nyepesi ambayo inapaswa itamkwe pamoja na kusadiki ili mtu aweze kuingia
katika Uislamu, kama ilivyoelezwa hapo juu. Ushahidi wa Imani ndio
nguzo muhimu zaidi katika Uislamu.
2) Swalah
Waislamu huswali Swalah tano kila siku. Kila Swalah huchukuwa muda
mfupi wa dakika chache tu. Swalah katika Uislamu ni mawasiliano ya moja
kwa moja kati ya mja na Mwenyezi Mungu. Hakuna kishenga baina ya
Mwenyezi Mungu na mfanyaji ibada.
Ndani
ya Swalah, mtu hujisikia ndani mwake furaha, amani na faraja, na
kwamba Allaah yu radhi naye. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) amesema: ((Bilaal adhini, ili tufarijike nayo.))[109] Bilaal alikuwa mmojawapo wa Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na alikuwa mwadhini.
Swalah
hufanyika wakati wa Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na ‘Ishaa.
Muislam anaweza kuswali karibu mahali popote, kama vile mashambani,
ofisini, viwandani au vyuoni.
Tafadhali, tembelea www.islam-guide.com/pillars kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya Swala katika Uislamu.[110]
3) Kutoa Zakaah (Kuwakunjulia Wenye Dhiki):
Kila kitu ni cha Mwenyezi Mungu, na hata mali zinazohifadhiwa na wanaadamu kama dhamana. Maana khalisi ya neno Zakaah ni
zote mbili ‘kutwaharisha’ na ‘kukua.’ Maana ya kutoa Zakaah ni kutoa
asilimia iliyotajwa bayana kutokana na mali fulani kwa kuwapatia
makundi fulani ya watu wenye dhiki. Asilimia inayopaswa kulipwa
kutokana na dhahabu, fedha na pesa taslimu zenye kufikia kiasi
kinacholingana na gramu 85 za dhahabu na kubaki katika miliki ya mtu kwa
mwaka mmoja wa Kiislamu ni asilimia mbili unusu. Tunavyovimiliki
hutakasika kwa kutenga pembeni sehemu ndogo tu kwa ajili ya wenyedhiki,
na kama vile kupogoa matawi ya mimea, huku kupunguza salio na kunatia
moyo wa ukuaji mpya.
Mtu anaweza kutoa zaidi kadiri atakavyo kama Sadaka.
4) Kufunga katika Mwezi wa Ramadhaan Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhaan,[111]Waislamu hufunga tangu Alfajiri hadi kuchwa kwa jua, kwa kujizuia kula, kunywa na tendo la ndoa.
Ingawa Swawm ni yenye faida za kiafya, huchukuliwa kimsingi
kuwa ni namna ya kuisafisha nafsi kiroho. Kwa mmojawapo kujizuia dhidi
ya starehe za kidunia, japo kwa muda mfupi, mfungaji hupata huruma ya
kweli kwa wanaopatwa na njaa, kadhalika na kuongezeka kwa maisha yake
ya kiroho.
5) Kuhiji Makkah:
Hija
ya kila mwaka Makkah ni faradhi ya kufanywa mara moja tu maishani kwa
wenye uwezo wa kimwili na mali katika kuitekeleza. Kadiri ya watu
milioni mbili huenda Makkah kila mwaka kutoka kila sehemu duniani.
Ingawa mara zote Makkah huwa imesheheni wageni, Hija ya mwaka hufanywa
katika mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya kiislamu. Mahaji wa
kiume huvaa nguo maalumu na rahisi ambayo huondosha mbali tofauti za
kimatabaka na tamaduni kiasi kwamba wote huwa sawa mbele ya Mwenyezi
Mungu.
Mahujaji wakiswali katika Msikiti wa Haram huko Makkah. Msikitini humu mna Ka’abah (jengo jeusi linaloonekana katika picha) ambalo Waislamu hulielekea wakati wakiwa katika Swalah. Ka’abah ni mahali pa ibada ambapo Mwenyezi Mungu Aliwaamuru Mitume Ibraahiym na mwanaye, Isma’iyl waijenge.
Ibada za hija ni pamoja na kuitufu Ka’abah mara saba na kwenda mchakamchaka baina ya kilima cha Swafa na Marwa mara saba, sawa na Hajar alivyofanya wakati akitafuta maji. Kisha, Mahujaji husimama pamoja katika uwanja wa ‘Arafah[112]na kumwomba Mwenyezi Mungu wakipendacho na kwa ajili ya maghufira, katika kile ambacho mara nyingi hufikirika kuwa ni onyesho la awali la Siku ya Malipo.
Mwisho wa Hijjah huweza kujulikana kwa sikukuu ya ‘Iydul-Adhw-haa,
ambayo husherehekewa kwa Swalah. Sikukuu hii na ‘Iydul-Fitwr, sherehe
ya kuadhimisha mwisho wa Ramadhaan ndio sikukuu mbili za kila mwaka
katika kalenda ya Kiislamu.
Tafadhali, tembelea www.islam-guide.com/pillars kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya nguzo tano za Kiislamu.
No comments:
Post a Comment